Psalms 137

Maombolezo Ya Israeli Uhamishoni


1 aKando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza
tulipokumbuka Sayuni.

2 bKwenye miti ya huko
tulitundika vinubi vyetu,

3 ckwa maana huko hao waliotuteka
walitaka tuwaimbie nyimbo,
watesi wetu walidai nyimbo za furaha;
walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja kati ya nyimbo za Sayuni!”


4 dTutaimbaje nyimbo za Bwana,
tukiwa nchi ya kigeni?

5 eNikikusahau wewe, ee Yerusalemu,
basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake.

6 fUlimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changu
kama sitakukumbuka wewe,
kama nisipokufikiri Yerusalemu
kuwa furaha yangu kubwa.


7 gKumbuka, Ee Bwana, walichokifanya Waedomu,
siku ile Yerusalemu ilipoanguka.
Walisema, “Bomoa, Bomoa
mpaka kwenye misingi yake!”


8 hEe binti Babeli, uliyehukumiwa kuangamizwa,
heri yeye atakayekulipiza wewe
kwa yale uliyotutenda sisi:

9 iyeye ambaye atawakamata watoto wako wachanga
na kuwaponda juu ya miamba.
Copyright information for SwhKC